Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza jinsi vipengele vya kitamaduni katika matini teule ya Kiswahili na Kikalenjin vilivyochangia mtafsiri kuiandika upya Bukuit ne Tilil. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili, ambazo ni nadharia ya tafsiri vitendo ambayo ilitumika kubaini jinsi tofauti za kimazingira kati ya hadhira ya matini asilia na ya matini pokezi ilivyopelekea uandishi upya kufanyika wakati wa kutafsiri. Nadharia ya pili ni ya ulinganifu,ambapo matini asilia ililinganishwa na matini pokezi ili kubai ni kama ujumbe ulihifadhiwa katika matini tafsiri.Aidha, tamaduni, matumizi ya msamiati na sarufi zililinganishwa kwa kuchunguza mikakati na mbinu zilizotumika kutafsiri matini asilia, na hivyo kubaini uandishi upya katika matini pokezi. Data zilikusanywa kupitia uchunguzi maktabani na vilevile kuwasaili washikadau katika Ofisi ya Utafsiri wa Bibilia ya Kapsabet na Shirika la Kutafsiri Biblia nchini, pamoja na wazungumza lugha ya Kikalenjin ambao walituelekeza juu ya matumizi ya baadhi ya maneno. Usampuli wa kimakusudi ulitumiwa ili kupata data iliyotumika katika uchanganuzi. Kitabu cha Mithali katika Agano la Kale kiliteuliwa kwa minajili ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa: utamaduni wa Waswahili na wa Wakalenjin ni tofauti na hii ilipelekea uandishi upya ufanywe katika tafsiri. Utafiti unapendekeza yafuatayo: Sera za elimu kuhusu lugha za kienyeji zinafaa kutilia maanani tafsiri ya matini za kufundishia.
scite is a Brooklyn-based organization that helps researchers better discover and understand research articles through Smart Citations–citations that display the context of the citation and describe whether the article provides supporting or contrasting evidence. scite is used by students and researchers from around the world and is funded in part by the National Science Foundation and the National Institute on Drug Abuse of the National Institutes of Health.
customersupport@researchsolutions.com
10624 S. Eastern Ave., Ste. A-614
Henderson, NV 89052, USA
Copyright © 2024 scite LLC. All rights reserved.
Made with 💙 for researchers
Part of the Research Solutions Family.